“Iliniuma sana baada ya kurudi na kukuta ujumbe ambao nilikuwa nimepewa maelekezo kwa ajili ya kumuona mhusika kusafiri na kuungana na wasanii wa nchi mbalimbali kwa ajili ya utengenezaji wa filamu na mimi muonekano wangu wa kipekee uliwavutia sana wazungu,”anasema.
Biggie anasema pamoja na kukosa nafasi hiyo kwa kuchelewa kuwasiliana na wahusika alijisikia vibaya lakini kwa sababu lengo lake ni kuwa msanii wa kipekee katika tasnia ya filamu kwa ukanda wa Afrika Mashariki na kati amekuwa makini sana anapopata nafasi kwa ajili ya kuigiza, ndio akiwa kama mhusika mkuu katika filamu ya Mdundiko ameweza kufanya makubwa na filamu hiyo kuibuka na ushindi nje ya nchi.
Filamu ya Mdundiko ilishinda tuzo ya hadithi bora ya asili katika tamasha kubwa la Silicon Valley African Film Festival (SVAFF 2013) sinema ya Mdundiko ilinyakua tuzo ya (Achievement Narrative in Feature Film) iliyotolewa katika jumba la sinema la San Antonio Circle Mountain View, katika Chuo cha Muziki na Sanaa California, Marekani.


0 maoni:
Chapisha Maoni