Kwa wale tuliokuwa na nia njema na
kijana Mnyika tumekuwa tukitumia juhudi sana kumuasa arudi shule akasome
lakini ushauri wetu haukuzingatiwa na mhusika.
kufuatia ukaidi wake huo, leo
amehadhirika kwa kukosa nafasi na fursa NONO zaidi kisa tu hana hata
stashahada (diploma) ukiachilia mbali shahaba ya kwanza.
Kwa ufupi ni kwamba - ndugu Mnyika
alikuwa miongoni mwa wajumbe ambao walitakiwa kuwa wenyeviti wa kamati
kwenye bunge la katiba kwa mujibu wa maoni ya wajumbe kadhaa.
Lakini kwa bahati mbaya maoni na mapenzi
ya wajumbe hao yaliyeyuka ghafla baada ya maamuzi ya kamati ya kanuni
kuweka kigezo cha shahada kama hitaji la kuwa mwenyekiti au makamu
mwenyekiti kwenye kamati za bunge maalumu la katiba.
Aidha, juhudi kadhaa zilifanywa na
wapenzi wa Mnyika kuweza kukipoteza kigezo cha shahada ili kisimzuie
Mnyika kuwa mwenyekiti wa kamati mojawapo ya bunge kati ya 12 zitakazo
undwa.
Lakini jitihada hizo za wapenzi wa
Mnyika hazikuzaa matunda hivyo kugonga mwamba baada ya mhe Simbachawene
kusisitiza kuwa hitaji la kuwa na shahada ili uwe mwenyekiti wa kamati
ni la kisheria.
Rai yangu: Kama Mnyika kweli ni kichwa
kama ambavyo anapambwa na baadhi ya mashabiki wake. Hivi kupata shahada
kuna ugumu gani kwake? Si arudi shule ili awe asset kwa taifa kuliko
huku kudhalilika kwake kwa kukosa shahada.
Source:Jamii Forums
Home
»
»Unlabelled
» DAH!! MNYIKA KAPOTEZA NAFASI MUHIMU SANA HIVIHIVI
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)


0 maoni:
Chapisha Maoni