KUFUATIA sintofahamu inayozuka kila kukicha ndani ya Bunge Maalum la
Katiba mjini Dodoma, mbunge mmoja wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania (jina tunalo) ameibuka na kumtaka Rais Kikwete ‘JK’ kulivunja
bunge hilo.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda Jumamosi iliyopita kwa sharti la
kutoandikwa jina lake gazetini, mbunge huyo kutoka Chama cha Mapinduzi
‘CCM’ ambaye kwa sasa ni mjumbe, alisema kuwa hali ilivyo sasa bungeni
kuna uwezekano mkubwa wa kutokuwepo kwa faida ya kikao hicho.
“Kila siku hili, mara lile. Watu wazima lakini mambo yao ni kama
watoto wadogo, mimi namshauri JK aamue kulivunja hili bunge halafu
mchakato wa rasimu ya katiba upelekwe kwa wananchi wakaupigie kura,”
alisema mbunge huyo akionesha jazba.
Aliendelea kuweka wazi kwamba kinachomshangaza wenye vurugu ndani ya
bunge hilo ni pamoja na wabunge wa zamani ambao hawatokani na wale 201
aliowachagua rais.
“Mimi nashangaa sana, tena wabunge wengine wenye vurugu ni wale
wazoefu si wale wajumbe wa JK, sasa tunakwenda wapi? Siamini kama kweli
hili bunge litakwenda hadi kumalizika,” alisema mheshimiwa huyo.
Home
»
»Unlabelled
»
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)

0 maoni:
Chapisha Maoni