Ismail Issa Makombe 'Mapembe' alivyo sasa.
Mapembe ambaye anapiga mzigo katika Kampuni ya Al-Riyam inayozalisha
kipindi cha vichekesho cha Vituko Show kinachorushwa kwenye Runinga ya
Channel Ten, amelia kuwa anateseka na ugonjwa huo tangu mwaka jana.
...Mapembe baada ya kuvimba tumbo.
Msanii huyo alifunguka kwamba alipimwa katika Hospitali ya Burhan,
Dar na kuambiwa kuwa mwili wake umejaa sumu kwa asilimia 93 na ini
limefeli huku akiwa ametokwa na vidonda usoni na tumbo lake kuvimba.
“Nimeamua kurudi nyumbani kwetu Mtwara ili angalau niombe msaada kwa
ndugu na jamaa zangu niweze kuishi na kujaribu kupata matibabu zaidi.
...Wakati akiigiza.
“Hali yangu ni mbaya sana kwani mwanzo
nilikuwa nikisaidiwa na bosi wangu ambaye naye kwa sasa anaonekana
kuelemewa na majukumu yake, hivyo nawaomba sana wadau waweze kunisaidia
kwa sababu ninaumia sana.
“Imefikia hatua leo ninatambua kuwa wasanii wa filamu ni wanafiki,
maana tangu mwaka jana hadi leo ninaumwa lakini hakuna hata mmoja
aliyeweza kunisaidia zaidi ya Kitale ambaye alikuja kuniona,” alisema.
...Mapembe akiwa hoi.
Mapembe kabla hajaugua alikuwa akiigiza kwenye Kundi la Vituko Show kwa kuvaa uhusika wa aina mbalimbali lakini mara nyingi alikuwa akifiti sana alipokuwa akiigiza kama askari wa usalama barabarani ‘trafiki’.Yeyote aliyeguswa na matatizo ya msanii huyu anaweza kumsaidia kwa kutumia fedha kwa Tigo Pesa kwa namba 0719 985659 au Airtel Money kwa namba 0784 328963.
gpl




0 maoni:
Chapisha Maoni