Mchungaji
Mtikila alisimama ghafla na kusema: Mwenyekiti kwanini unaninyima haki
yangu ya kuzungumza, nataka kujua kwanini unaninyima haki ya kuzungumza.
Kuzungumza ni haki yangu.”
Mchungaji
Mtikila amezungumza kwa jazba huku wajumbe wengine wakimzomea, lakini
bila uwoga aliendelea kuzungumza na kusema yanayofanyika Mungu anapenda
na yeye ana amini katika Mungu, lakini “Wewe Mwenyekiti inaonekana kuwa
hupendi Mungu.”
Wakati
Mchungaji Mtikila akimwakia Kificho, Felix Mkosamali alilipuka na
kumwambia mwenyekiti kuwa tangu jana pia anamnyima nafasi.


“Ninyi mmejipanga, kupitisha kanuni mbovu, alafu sisi wengine hamtupi nafasi,” amesema Mkosamali.
Mwenyekiti Kificho aliwajibu kuwa kwa bahati mbaya wamekosa nafasi na hivyo wawe wavumilivu.
Kificho
anatangaza utaratibu wa kumchagua Mwenyekiti wa kudumu wa Bunge na
wajumbe wanaotaka kugombea nafasi hiyo wametakiwa kuchukua fomu ya
kugombea.
Bunge hilo limeahirishwa mpaka kesho na kanuni zitaanza kufanya kazi rasmi.
0 maoni:
Chapisha Maoni