Joseph Shaluwa na Erick Evarist
SETH Bosco aliye mdogo wa marehemu
Steven Kanumba, aliyekuwa staa wa filamu za Kibongo, ameibuka na kueleza
mambo ya kushangaza, akidai kaka yake huyo amekuwa akimtokea ndotoni.
Seth ndiye msimamizi na mwendeshaji wa
Kampuni ya Kanumba The Great Film baada ya kifo cha Kanumba kilichotokea
Aprili 07,2012 nyumbani kwake, Sinza – Vatican, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari hizi,
wikiendi iliyopita jijini Dar es Salaam, kwa sauti ya huzuni, Seth
alisema: “Kiukweli sina amani, hii hali inanitesa sana. Kila mara
ananitokea ndotoni na kunieleza mambo yanayofanana.”
MAMBO GANI?
“Analalamika kwa nini eti ofisi yake
aliyoiacha haina mafanikio. Sasa nashindwa kuelewa, ni mafanikio gani
anayozungumzia. Analalamika kwa nini filamu hazitolewi, ni jambo la
kweli lakini lipo nje ya uwezo wangu,” alisema Seth.
AMANI: Anakutokea kivipi yaani?
SETH: Nikiwa usingizini, nakuwa kama
naota, lakini mazungumzo yanakuwa ya moja kwa moja... ndoto ikikatika,
nashtuka na kujikuta nahema kwa kasi.
AMEMTOKEA MARA NGAPI?
“Mara ya tatu sasa, ndiyo maana
nimeshindwa kuvumilia. Kinachonishangaza ni kwamba, kila anaponitokea,
lazima nishtuke mwishoni na lazima niheme kwa kasi na kutoka jasho
jingi.
“Mwanzoni nilichukulia kawaida, lakini
alivyonijia mara ya pili na ya tatu nikaona hili suala siyo la kulikalia
kimya, ikabidi nimwambie mama.”
MAMA KANUMBA ANASEMAJE?
“Mama alishtuka na ameshangazwa sana na
hali hiyo. Ameniuliza imenitokea mara ngapi, nikamwambia tatu, akasema
lazima tufanye maombi kuondoa hali hiyo,” alisema Seth huku akionesha
uso wa wasiwasi.
Home
»
»Unlabelled
» MDOGO WAKE KANUMBA AIBUKA NA KUFUNGUKA HAYA
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)


0 maoni:
Chapisha Maoni