STAA
nguli wa muziki wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila,’’Ray C’ amefunguka
kuwa alipopata matatizo kipindi alipokuwa akitumia madawa ndipo
alipogundua rafiki wa kweli na wa uongo ambapo wengi aliowachukulia kama
ndugu ndiyo walikuwa wa kwanza kumkimbia na wale aliokuwa awategemei
ndiyo waliokuwa mstari wa mbele kumsaidia japo kwa ushauri.Kupitia
account yake ya instagram Ray C aliandika ‘’Nilipopata matatizo ndio
niligundua rafiki wa kweli na rafiki waongo kwani wengi niluowachukulia
kama ndugu ndio walikuwa wa kwanza kunikimbia na wale niliokuwa
nisiowategemea ndio walikuwa mstari wa mbele kunisaidia japo ushauri.Usiyemdhania
ndiye…..wanaokuumiza ni wale walio karibu yako siku zote so guys be
very careful na watu wa karibu wanaojua kila kitu chako! na hao ndio
wanaoweza hata kukudhuru..
0 maoni:
Chapisha Maoni