Waziri
wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mjumbe wa Bunge Maalumu la
Katiba,ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Urambo Mashariki,Mh Samwel Sitta
ameibuka kinara kwenye nafasi aliyowania ya kuwa Mwenyekiti wa Bunge
Maalum la Katiba mara baada kumbwaga mpinzani wake,Wakili wa
Kujitengemea Ndugu Hashim Rungwe,Sitta anaibuka kinara na kuichukua
nafasi hiyo ya kuwa Mwenyekiti wa Kudumu wa Bunge hilo Maalum la Katiba
kufuatia Mwenyekiti wake wa Muda,Mh Ameir Pandu Kificho,ambaye mda wake
wa kuliendesha bunge hilo unakoma leo.
Jumla
ya Kura zilizopigwa ni 563 na zilizoharibika ni 7,kufuatia idadi hiyo ya
Kura Ndugu Hashim Rungwe amepata kura 69 na Mh.Samwel Sitta ameibuka na
kura 487,kwa Matokeo hayo imetangazwa kuwa Mh.Samwel Sitta ndiyo
mshindi.
0 maoni:
Chapisha Maoni