Shabiki
wa Timu ya Yanga SC, Deodatus Isaya Lusinde, mkazi wa Kipunguni A,
amefariki dunia jana jioni baada ya kuanguka ghafla wakati
akishangilia bao la Yanga lililofungwa na Didier Kavumbagu katika dakika
ya 14 kipindi cha kwanza.
Marehemu
amepoteza maisha akiwa chumba cha matibabu mara baada ya kuwekewa
mashine ya oksijeni na taarifa kuhusu kifo cha shabiki huyo
zimethibitishwa na mmoja wa madaktari aliyemhudumia akiwa uwanjani kabla ya mauti kumfika, Nassor Matuzya.
Bwana
Isaya alikuwa Meneja wa Bar ya Rose Hill iliyopo Segerea jijini Dar.
Ameacha mke aitwaye, Rose William Lusinde ambaye ni askari magereza.
Marehemu
amekutwa na mauti hayo wakati wa mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, kati
ya timu yake ya Yanga na Azam, mchezo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.


0 maoni:
Chapisha Maoni