About

www.facebook.com/archileusanatory/pambazuabongo


KWA miaka mingi sasa, baadhi ya watu wamegubikwa na dhana potofu ya kwamba, kuwa mweupe ndiyo urembo .

Dhana hii imewafanya wengi waanze kutumia vipodozi vikali, bila kujali madhara ya baadaye.
Kwa mfano, hata baadhi ya wasanii, wake kwa waume, wamekuwa wakijibadili ngozi zao na tumewaona wakibadilika hatua kwa hatua.
Hata hivyo, unapohisi kuna uzuri, mara nyingi kuna kudhurika. Madhara ya awali ya vipodozi hivi, huonekana kwa mtumiaji kubabuka ngozi, kuwa na mabaka meusi au ngozi kuwa nyekundu. Lakini yapo madhara mengine mabaya zaidi ya hayo.
Kemikali hatari
Katika bidhaa hizo zinazotumika za kujichubua, kuna kemikali za aina mbili.
Kwanza ni ‘Hydroquinone’ na ya pili ni ‘Mercury’.
Hydroquinone kemikali hii ni sumu kali, ambayo hutumika kwa ajili ya kuchapisha picha na kutengeneza bidhaa za mpira.
Hutumika pia kama kisaidizi katika kutengeneza rangi za nywele.Mercury nayo ni kemikali ya sumu inayoweza kuuzwa katika maduka ya madawa tu tena maelekezo ya daktari...

0 maoni:

Chapisha Maoni

 
Top