BABA wa msanii wa Bongo Fleva, Nasibu
Abdul ‘Diamond’, Abdul Jumaa amefunguka kuwa mwanaye huyo siyo riziki
yake kwani hana dalili zozote za kumjali kama mzazi.
Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Akistorisha na gazeti hili, mzee huyo
alisema kwa sasa hataki kumzungumzia kabisa Diamond kwa sababu
alishamtumia ujumbe kwamba anatakiwa kubaki kama baba tu na si
vinginevyo.
'Mshua' Nasibu Abdul ‘Diamond’, Abdul Jumaa.
“Sitaki kumzungumzia Diamond kabisa kwa
sababu nitaonekana najipendekeza kwake kwa sababu ameshasema nibaki kama
baba tu, naona siyo riziki yangu,” alisema baba Diamond.
Alipoulizwa Diamond kuhusiana na maelewano hafifu na baba yake, alijibu: “no comment.”
-GPL
0 maoni:
Chapisha Maoni