Star wa Bongo fleva Diamond Platnumz
amesema kuwa siku chache kabla mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi
Maalim Muhidin Gurumo hajaaga dunia alikuwa amemuandikia wimbo kama
shukrani kwa kumpa zawadi ya gari mwaka jana.
Diamond alimzawadia mzee Gurumo gari mpya mwaka jana wakati wa uzinduzi wa video yake ya ‘Number 1’.
Platnumz amesema meneja wake Babu Tale
alimpa taarifa hiyo njema ya kuandikiwa wimbo na Gurumo lakini kwa
bahati mbaya mzee Gurumo alifariki kabla hajamkabidhi wimbo huo.
“Juzi kampigia simu Tale akamwambia kuna
nyimbo nimemtengenezea Diamond kwasababu kwa alichonifanyia mimi
nimeshukuru sana cha kumlipa mimi sina lakini nimemuandikia nyimbo”
amesema Platnumz kupitia 255 ya XXL ya Clouds Fm.
“so alikuwa anamwambia Tale kama
ameniandikia nyimbo, so angependa anipatie nikamwambia sawa. Kama siku
tatu hivi nyuma, jana ndio nasikia taarifa hizi so najiona kama
nimechanganyikiwa hivi.”
Platnumz ameongeza kuwa mara ya mwisho
kuonana na Gurumo ilikuwa ni takribani wiki tatu zilizopita baada ya
mwimbaji huyo mkongwe kumsurprise kwa kuhudhuria katika show aliyokuwa
anatumbuiza Diamond kwa lengo la kutaka kumwona na kumshukuru kwa zawadi
ya gari aliyompatia.
“Mara ya mwisho kukutna naye nilikuwa
nafanya show Coco akaja maskini ya Mungu mpaka kwenye show…kama wiki
moja nyuma kama sikosei au wiki mbili. Akaja akasema nimekuja hapa
kukuona, alipenyapenya hadi akaweza kufika pale…nilivyomuona anakuja
ilibidi pale nikatishe show nikamsalimia kidogo halafu nikaendelea na
show, halafu baadae nikawa niko nae backstage na nini nikazungumza
nae.So akasema nimekuja kukushukuru sana sana sana, akasema ningependa
uje nyumbani nikamwambia sawa.”Amesema Diamond.
Mwili wa marehemu mzee Gurumo umepelekwa
kijijini kwake Masaki, wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani kwaajili ya
mazishi yanayofanyika leo.
Bongo5
Home
»
»Unlabelled
» KABLA GURUMO HAJAFARIKI ALIMWANDIKIA DIAMOND WIMBO KAMA ZAWADI
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)


0 maoni:
Chapisha Maoni