Rubani msaidizi wa ndege iliyopotea
namba MH370 alipiga simu yake ya mkononi wakati ndege ikiruka chini
chini kupita pwani ya magharibi mwa Malaysia.
Wachunguzi wamegundua kwamba simu hiyo
ilipigwa kutoka kwenye simu ya mkononi ya Fariq Abdul Hamid wakati
Boeing 777 ikiruka chini chini karibu na kisiwa cha Penang, kaskazini
mwa pwani ya magharibi ya Malaysia.
Gazeti la The New Straits Times
limeripoti leo kwamba ilifahamika ndege hiyo, ilikiwa na watu 239 ndani
yake, ilikuwa ikiruka chini chini kiasi cha minara ya mawasiliano
iliyokuwa karibu kuweza kunasa ishara za Fariq.
Simu hiyo ilikatika ghafla, hata hivyo
imefahamika kwamba mawasiliano yalirushwa na kituo kidogo cha
mawasiliano kilichopo kwenye jimbo la Penang.
Gazeti hilo lilisemwa kwamba haikuweza
kujulikana mara moja Fariq alikuwa akimpigia nani 'kutokana na chanzo
cha habari kutotaka kuweka bayana taarifa zaidi za uchunguzi.'
Liliongeza: "Mnara wa kampuni ya mawasiliano ulinasa simu hiyo aliyokuwa akijaribu kupiga.
"Kuhusu kwanini simu hiyo ilikatika,
inawezekana sababu ndege hiyo ilikuwa ikienda kwa kasi mbali na mnara
huo na haikuweza kupata mawasiliano kwenye mnara unaofuatia," gazeti
hilo lilisema, likinukuu vyanzo vya habari.
Gazeti hilo liliongeza kwamba imebainika
pia kwamba mawasiliano ya mwisho ya Fariq yalikuwa kupitia WhatsApp na
kwamba yalifanyika majira ya Saa 5:30 usiku wa Machi 7, muda mfupi kabla
hajapanda ndege hiyo kuanza safari ya masaa sita kwenda Beijing, China.
The New Straits Times lilisema
lilielezwa kwamba ukaguzi wa kumbukumbu kwenye simu ya Fariq ulionesha
kwamba mtu wa mwisho kabisa kuongea naye ilikuwa 'mtu wake wa kawaida
(namba iliyokuwa ikijirudia rudia katika orodha ya simu zake
alizopiga).'
Simu hiyo ya mwisho, lilisema gazeti
hilo, ilipigwa sio zaidi ya masaa mawili kabla ya ndege hiyo kuruka saa
6:41 usiku wa Machi8 kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kuala
Lumpur.
Vyanzo tofauti vililieleza gazeti hilo
kwamba ukaguzi kwenye simu ya Fariq ulionesha kwamba mahusiano na simu
hiyo aliyopiga simu hiyo ya mwisho kabla ya kupanda ndege hiyo yalikuwa
'adilifu'.
"Hii ni matokeo ya kawaida kwa simu hiyo kuwa imezimwa.
"Wakati fulani, hatahivyo, wakati ndege
hiyo ikiwa angani, kati ya Igari na eneo hilo karibu na Penang (muda
mfupi kabla ya ndege hiyo kupotea kwenye rada), laini hiyo
'iliunganishwa tena'."
Gazeti hilo lilisema kwamba
uunganishwaji haumaanishi kwamba lazima simu hiyo kwamba ilipigwa.
Inawezekana pia ni matokeo ya simu hiyo kuwa imewashwa tena.
Jana ilionekana kama kisanduku cheusi kinaweza kuwa kimepatikana chini katika Bahari ya Hindi.
Kituo cha redio cha 6PR kilituma ujumbe
katika twitter ugunduzi huo, kikimnukuu mtaalamu wa anga Geoffrey
Thomas, ambaye alibainisha kinasa taarifa hicho cha ndege hiyo hatimaye
kimepatikana zaidi ya mwezi mmoja baada ya Boeing 777 kupotea.
Waziri Mkuu wa Australia Tony Abbott,
ambaye yuko nchini China, alisema watafutaji wana 'uhakika' ishara hizo
zilizopatikana zilikuwa kutoka kwenye kisanduku cheusi kutoka kwenye
ndege ya MH370.
"Hakika sitaki kusema taarifa zaidi ya hapo kwa wakati huu... kama ishara ya heshima kwa watu wa China na familia zao."
Home
»
»Unlabelled
» MAPYA YAIBUKA NDEGE ILIYOPOTEA, RUBANI ALIPIGA SIMU ANGANI
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)


0 maoni:
Chapisha Maoni