Emmanuel Okwi.
Achana na hao njoo Simba, ukichukua fungu la dola
4,000 sawa na Sh 6.4 milioni za Kitanzania anazolipwa fowadi huyo
zinatosha kulipa mishahara ya wachezaji watatu muhimu wa Msimbazi,
Amissi Tambwe, Joseph Owino na Ramadhani Singano ‘Messi’.
Kiasi hicho anacholipwa Okwi ni zaidi ya fedha
aliyokuwa akilipwa pia mshambuliaji wa zamani wa Simba, Felix Sunzu
ambaye alikuwa analipwa Sh 5 milioni kwa wakati huo akiwa ndiye mchezaji
pekee ghali kuliko wote.
Mshambuliaji huyo wa Yanga raia wa Uganda
alisajiliwa na mabingwa hao wa soka nchini wakati wa usajili wa dirisha
dogo akitokea SC Villa ya Uganda baada ya kutofautiana na timu yake ya
Etoile du Sahel ya Tunisia alikouzwa na Simba msimu uliopita.
Usajili wa Okwi ulileta utata mkubwa ambao
ulisababisha akose baadhi ya mechi mpaka ulipotolewa ufafanuzi kutoka
Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kwa kile kilichokuwa kinadaiwa
kuwa ana mkataba na Etoile du Sahel.
Hivi sasa Okwi ameonekana kuanza usumbufu ndani ya
klabu hiyo baada ya kudaiwa kuondoka kambini bila ya kutoa sababu za
kufanya hivyo huku akiwa ameifungia Yanga mabao matatu pekee tangu
ajiunge nayo.
Mbali na mchezaji huyo wachezaji wengine
wanaofaidi mishahara minono kutoka Azam FC ni Kipre Tchetche, Kipre
Balou, John Bocco, Agrey Morris, Briany Omony na Haruna Niyonzima wa
Yanga ambao wanapata Sh 4 milioni.
Beki Mbuyu Twite wa Yanga yeye anapata Sh 3.6
milioni huku beki wa Simba Joseph Owino ndiye anayeingiza fedha ndefu
ndani ya klabu hiyo kwa kupokea mshahara wa dolla 2,000 sawa na Sh 3.2
milioni.
Yanga imeonekana kuwafunika wachezaji wa Simba
kwani wachezaji wake wengi wanapata mishahara ya kuanzia Sh. milioni
moja kupanda juu huku wachezaji wa Simba wengi wao wakianzia shilingi
milioni moja kushuka chini.
Mwanaspoti limebaini kuwa wachezaji wazawa hakuna
anayelipwa mshahara wake zaidi ya Sh 5 milioni walio wengi mishahara yao
haizidi Sh 1 milioni ingawaje wachache wamefikisha Sh 4 milioni.

0 maoni:
Chapisha Maoni