Kamati kuu ya chama cha mapinduzi (CCM), imekutana mjini Dodoma chini ya Mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete, na kutoa tamko la kulaani kitendo cha wajumbe wa Bunge maalum la katiba, wanaounda kundi la umoja wa katiba ya wananchi (ukawa), kususia vikao vya bunge hilo, na kudai kuwa kundi hilo linakiuka katiba na halina nia wala dhamira ya kuhakikisha katiba mpya inapatikana
Akitoa taarifa kuhusu kikao hicho cha dharura cha siku moja, Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, Nape Nnauye, amesema kikao hicho kimepokea taarifa ya yaliyojiri ndani na nje ya bunge la katiba, ambapo imesikitishwa na baadhi ya wajumbe wa bunge hilo kususia kikao hicho na kwenda kupotosha ukweli kwa wananchi wakati muda wa kupeleka rasimu ya katiba kwa wananchi bado haujafika
Nape ameongeza kuwa, CCM itaendelea kulinda maslahi ya nchi, na
kuhakikisha umoja na mshikamano wa nchi unadumishwa kwa gharama yeyote
ile, na itajibu kila uchochezi unaoonyeshwa na baadhi ya watu, kwa
maslahi yao binafisi kwa kuwaeleza watanzania Ukweli
Eatv
Eatv

0 maoni:
Chapisha Maoni