Wa kwanza ni Afisa Usalama wa Taifa
Mwandamizi, Silvanus Adriano Mzeru (56) aliyeuawa kwa kupigwa risasi na
watu wasiojulikana Aprili 29, mwaka huu maeneo ya Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar.
Gazeti hili lilifuatilia habari hiyo na
kunasa madai kwamba wauaji hao walikuwa na pikipiki aina ya Boxer.
Ilielezwa kuwa wadunguaji hao walimfuatilia afisa huyo tangu maeneo ya
Tazara jijini Dar.
Ilidaiwa kuwa, kufika eneo hilo la uwanja wa ndege, taa za kuongozea magari zilionesha ishara ya magari yanayotokea mjini yanatakiwa kusimama lakini baada ya dakika kama mbili taa hizo ziliruhusu magari kuondoka.

Ndipo ghafla watu hao waliokuwa
wamejibanza sehemu walimmiminia risasi marehemu upande wa mbele wa
kioo na kumfanya apoteze uelekeo na gari lake aina ya Toyota Land
Cruiser lenye namba za usajili T 844 CUG kwenda kuligonga kwa nyuma
gari lingine lenye namba T 786 BLS.
“Cha ajabu sasa, baada ya kufanya
kitendo kile, wale watu kwanza walipiga risasi hewani ili raia
wasisogelee eneo la tukio. Halafu ndani ya gari la marehemu walikuta
pesa ambazo kiwango chake hakijafahamika na ‘brifkesi’ inayodaiwa
ilikuwa na nyaraka mbalimbali,” kilisema chanzo.
Ukiachana na mauaji ya afisa usalama huyo, mfanyakazi mwingine wa ikulu, Rashid John Chilwangwa (45) naye alikutwa na mauti baada ya kuanguka ghafla.
Ukiachana na mauaji ya afisa usalama huyo, mfanyakazi mwingine wa ikulu, Rashid John Chilwangwa (45) naye alikutwa na mauti baada ya kuanguka ghafla.
Chilwangwa alifariki dunia ghafla saa
4:20, Mei Mosi, 2014 ndani ya Uwanja wa Uhuru wakati sherehe za siku ya
wafanyakazi duniani zikiendelea.
Waandishi wa habari walikuwepo katika
eneo la tukio na kushuhudia wafanyakazi wa ikulu na wananchi wengine
wakitokwa machozi mara baada ya kupokea taarifa za kifo hicho kutoka
kwa wafanyakazi wa Msalaba Mwekundu waliokuwa wakijaribu kuokoa uhai
wake.
Baadaye ilidaiwa kuwa, marehemu alikuwa akisumbuliwa na kisukari na siku ya tukio, presha yake ilipanda.
Baadaye ilidaiwa kuwa, marehemu alikuwa akisumbuliwa na kisukari na siku ya tukio, presha yake ilipanda.
Mwili
wa Chilwangwa uliagwa Ijumaa iliyopita nyumbani kwake, Mabibo jijini
Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo mke wa rais,
mama Salma Kikwete ( pichani).Marehemu Chilwangwa alizikwa Ijumaa hiyohiyo, Kisarawe, Pwani huku marehemu Mzeru akizikwa Mei 3, mwaka huu kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Mungu azilaze pema peponi, roho za marehemu hao. Amina.
cHANZO jPl
cHANZO jPl

0 maoni:
Chapisha Maoni