Tukio hilo limetokea jana Juni 30 majira ya saa 9 alasiri ambapo basi la abiria mali ya kampuni ya Lushanga lenye namba za usajili T 312 ATA likiwa na Abiria likitokea Mkoa wa Geita kuleleka mkoani Mwanza kupitia kivuko cha Kamanga.
Marehemu alikuwa anaendesha troli lililokuwa limebeba miti ambapo amepasuka kichwa na kusababisha Ubongo kutoka nje, na mwili wake umepelekwa katika hospitali teule ya wilaya ya Sengerema kwa ajili ya uchunguzi zaidi pamoja na majeruhi kwa ajili ya matibabu.
Kwa upande wa mashuhuda abiria waliokuwa katika basi hilo hakuna aliyejeruhiwa katika ajali hiyo pamoja na gari hilo kuharibika baada ya kushindwa kuendelea na safari hivyo kurudi nyuma na kujikita kwenye mtaro.
Hadi tunaandika habari hii chanzo cha ajali hii hakijajulikana kutokana na uchunguzi wa polisi wilayani humo kuhusu ajali hiyo kuendelea na dereva wa basi hilo na konda wake waliotokomea kusikojulikana kutokana na mkusanyiko wa watu eneo la tukio.




0 maoni:
Chapisha Maoni