MWISHONI mwa wiki iliyopita, taarifa
zilienea katika mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya habari Bongo
kwamba msanii wa Bongo Fleva, David Genzi ‘Young Dee’ na nyota wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’
wamebambwa na polisi wa doria wakivunja amri ya sita ndani ya gari
aina ya Hyundai, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam, tukio lililojaa utata
mkubwa.
Kwa mujibu wa habari hizo, wawili
hao walinaswa wakifanya uchafu huo na askari waliokuwa doria lakini wakawavuta
chobingo na baada ya muda, wakawaachia na kutokomea kusikojulikana.
Ili kupata ukweli wa tukio hilo la
aibu, paparazi wetu alianza kwa kumvutia waya Young Dee na kumsomea mashtaka
yake ambapo alifunguka kuwa ni kweli amezisikia habari hizo lakini akakana
kwamba ishu hiyo siyo ya kweli bali imezushwa na kundi la watu wenye lengo la
kumharibia jina lake mbele ya jamii.
“Siyo kweli kabisa, isitoshe
nina kama mwezi mzima sijaonana na huyo Lulu, huku ni kutaka kuchafuliana
majina tu,” alisema Young D.
Habari zinadai kuwa licha ya Young
Dee kukanusha kuwa hajaonana na Lulu kwa muda mrefu, siku ya tukio walikuwa
pamoja ingawa hawakutaka kuonekana na mtu yeyote.
Kwa upande wa Lulu alipotafutwa,
alifunguka: “Kweli nimesikia ishu kama hiyo ila kinachonishangaza na
kunisikitisha ni kwamba siku hiyo ya tukio inayotajwa mimi nilikuwa nyumbani na
siku nzima sikutoka kwenda popote, hata hiyo Mbezi iliyotajwa mimi siielewi
kabisa, hata lile gari mimi sina gari la aina hiyo wala sijawahi hata kulipanda
gari hilo na huyo Young Dee nina muda mrefu sana sijaonana naye,”
“Usiku wa kuamkia leo nilimpigia
mtangazaji mmoja ambaye aliirusha habari hiyo redioni, nikataka kujua ameipata
wapi habari hiyo? Akanijibu kwamba amepata tetesi tu. Sasa kama ni tetesi kwa
nini asichunguze kabla hajanichafulia jina?”
“Pia alisema kuna askari wa doria
walitukamata, nikamtaka anipeleke hicho kituo cha polisi tulikopelekwa ili
tuthibitishe kama ni kweli maana ishu hii inanichafua mimi na familia yangu,
akashindwa kufanya hivyo.
“Yaani naomba ieleweke kuwa
sijafumaniwa na siwezi kufumaniwa na mtu kama Young Dee maana kwanza hata
sijawahi kukutana naye hivi karibuni, sipendi kuchafuliwa na haya yote
namuachia Mungu atawajibu wote wanaonizushia,” alisema Lulu.

0 maoni:
Chapisha Maoni