Hayo yalielezwa na Mtaalamu wa Sheria ambaye pia
ni mmoja wa Wajumbe wa Kamati iliyoboresha Rasimu ya Kanuni zinazoongoza
Bunge hilo, Dk. Tulia Ackson, wakati akitoa ufafanuzi wa kanuni kwa
wabunge bungeni.
“Makatazo yanayopatikana katika kanuni ya 46.-(1)
ni kusema uongo, kutumia majina ya waasisi na marais kwa dhihaka,
kuzomea na kupiga kelele na mengine kama yanavyoonekana kwenye ibara
hiyo, hivyo ni vizuri kuhakikisha tunazingatia kanuni ili twende sawa
wakati wa mijadala,” alisema.
Pamoja na kuelezea vipengele vingine vilivyo
katika ibara hiyo, Dk. Ackson alisema mjumbe anapewa kinga na kanuni
hizo juu ya alichosema ndani ya mijadala bungeni, ikiwa amefanya rejea
katika kumbukumbu rasmi.
“Ikiwa mjumbe anazungumza, mjumbe mwingine
akafuata taratibu za kutoa taarifa. Atakaporuhusiwa na mwenyekiti wa
Bunge na ikaelezwa kuwa kinachoelezwa na mzungumzaji ni uongo,
mzungumzaji atapata muda wa kujibu madai yaliyotolewa dhidi ya
mazungumzo yake,’ alisema.
Kwa mujibu wa Dk. Ackson, kanuni zinaeleza kuwa
mzungumzaji atatakiwa kuthibitisha alichoeleza kuwa ni sahihi na kwamba
akishindwa kufanya hivyo, itachukuliwa kuwa amesema uongo na atastahili
adhabu husika.

0 maoni:
Chapisha Maoni