Alhamisi ya March 20 2014 lilitoka tamko ambalo lina maamuzi ya
msanii wa bongofleva Dogo Janja kuhusu kuomba msamaha na kuhitaji kurudi
kwenye kundi lake za zamani la Tiptop connection na kuyasahau
yaliyopita kati yake na aliyekuwa meneja wake pia ambae ni Madee.
Stori hii ina
pande nyingi sana ambazo zitazungumza kupitia hapahapa kwenye tovuti hii
lakini kwa kuanzia, baba mzazi wa Dogo Janja amepata nafasi kuzungumza
kwa mara ya kwanza baada ya mtoto wake kuomba msamaha.
Anasema
>>’Dogo Janja alishakua mtu mzima na tayari nilishawahi kumwambia
achague mahali atakapoona kuna manufaa kwake, akishafanya
maamuzi yake huwa ananishirikisha kwenye kujadiliana, tayari alishawahi
kuniambia kuwa atafanya maamuzi baada ya kuona Mtanashati hakuna
muelekeo wowote na hakuna anachopata ndipo akaniambia baba mimi mtu
yoyote au kundi lolote nitakalokubaliana nalo basi nitafanya nao kazi’.
Hayo ni maelezo ya Baba mzazi wa Dogo Janja ambae ametoa baraka zote
kwa Janja kurudi kujiunga na Tiptop Connection hivyo kazi imebaki
kusikia kutoka upande wa Tiptop kufahamu kama wameukubali msamaha wa
Dogo Janja.
Source: Milard Ayo
Home
»
»Unlabelled
» BAADA YA DOGO JANJA KUOMBA MSAMAHA NA KUTAKA KURUDI TIP TOP HII NDIYO KAULI YA BABA YAKE MZAZI JUU YA SWALA HILO..!!
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)


0 maoni:
Chapisha Maoni