About

www.facebook.com/archileusanatory/pambazuabongo

Kitunguu ni kiungo kinachotumika pia kama dawa ya Asili kwa kuwekwa kwenye chakula au mboga au hata kachumbari…Na …Kitunguu maji si kiungo pekee bali hufungua hamu ya kula chakula, hutuliza, hutia kiu, na hulainisha tumbo. Na huzidisha nguvu za kiume iwapo kitachemshwa.
Kazi kubwa ya mboga mboga viungo na matunda ni kulinda na kurekebisha mifumo mbalimbali ya ufanyaji kazi iliyoharibika mwilini.

Uharibifu huu unasababishwa na uchafu wa mazingira, uchovu wa mwili husababisha kuingia kwa wadudu wasiotakiwa mwilini kama vile virus na bacteria.

Wakati mwingine mifumo ya ufanyaji kazi wa mwili huharibiwa na sumu kutoka kwenye madawa ya kuulia wadudu wa majumbani kwa maana ya inzi, mende kombamwiko n.k.

Sumu ya mbolea zenye kemikali nyingi, na madawa makali ya kuulia wadudu waharibifu katika kilimo inaharibu sana mifumo ya ufanyaji kazi mwilini kwa sababu sumu hizi huchukua muda mrefu kuisha mwilini.

Mboga mboga zinazosaidia kurekebisha mifumo ya mwili hazishikiki siku tatu zimeota subhaanallah. Kuna mtaalam mmoja Aliniambia ukinunua mboga chagua zenye vitobo vitobo zilizoliwa na wadudu kwa sababu kemikali zinazowekwa katika mbolea hata wadudu wanaogopa sumu ya kemikali za mbolea siku hizi.

Tunatumia mbogamboga na matunda kama dawa au kinga kwa matatizo fulani.
Ni lazima unapotumia mbogamboga na matunda uweke nia ya kufanya hivyo na kufuata taratibu zake kwani  kila jambo linahesabiwa kwa nia. 

Kumbuka tu kuwa mwili una namna yake ya kujitibu na kujikinga.

Kitunguu ni kiungo kinachotumika pia kama dawa ya Asili kwa kuwekwa kwenye chakula au mboga au hata kachumbari.

Kitunguu maji si kiungo pekee bali hufungua hamu ya kula chakula, hutuliza, hutia kiu, na hulainisha tumbo. Na huzidisha nguvu za kiume iwapo kitachemshwa.

Kuna Aina kama tatu za vitunguu maji. Kuna vile vyeupe vyekundu na vya njano. Aina nzuri sana ni vitunguu vyeupe.

Kitunguu kina protini kiasi na kimejaa madini ya calcium na riboflavin kwa wingi sana.

Wenyewe wanasema kwa kila gram 100 kuna maji maji 86.6% protini 1.2% mafuta 0.1% nyuzinyuzi 0.6% wanga 11.1% madini mengine yaliyomo ni pamoja na phosphorus, chuma, carotene, thiamine, niacin na vitamin C.

Kwa tatizo la TB.

Juisi ya kitunguu ikitumika kijiko cha chai asubuhi na jioni inaondoa tatizo hili changanya na sukari guru.

Matatizo kwenye njia ya hewa (upumuaji).

Kitunguu kinayeyusha mgando kwenye mishipa ya damu na kuzuia isikae kwenye njia ya hewa. Hivyo hutibu kikohozi mafua na matatizo ya kwenye mapafu. Vijiko vidogo vitatu vya juisi yake, vilivyochanganywa sawa sawa na asali mara mbili kwa siku ni dawa tosha.

Pumu:

Changanya juisi ya kitunguu na asali halafu Atakunywa kiasi cha kikombe Asubuhi na jioni atafanya hivyo kwa muda wa mwezi mmoja tiba hii ni mujarrab.

Vitunguu vina madini ya chuma yanyoyeyuka kirahisi sana mwilini kwa hiyo ni vizuri kutibu ukosefu wa damu. Kwa mvilio wa damu Utachanganya juisi yake na mafuta ya kafuri utasugua mahala pa mvilio Asubuhi na jioni pamoja na kuacha kukipa kazi nzito kiungo chenye ugonjwa.

Magonjwa ya moyo.

Kwa kuwa kitunguu kina mafuta asili, madini mbalimbali pamoja na vitamini kadhaa kinasaidia kuondoa sumu zinazoweza kuudhuru moyo na hivyo kuondoa mchafuko kwenye mishipa ya damu.

Maji meupe jichoni.

Atatia jichoni matone ya Asali iliyochanganywa na maji ya kitunguu tiba hii ni mujarrab.

Kunyonyoka nywele.

Chukua maji ya kitunguu na usugulie ngozi ya kichwa kabla ya kulala Asubuhi utaosha kwa maji yenye uvuguvugu utakariri mpaka ugonjwa huo ukome.

Magonjwa ya meno.

Kutafuna ganda moja la kitunguu kwa siku huuwa vijidudu vibaya kinywani na kwenye meno.

Kitunguu kinatibu magonjwa mengi zaidi ya haya.

0 maoni:

Chapisha Maoni

 
Top