Mjumbe wa Kamati ya Kanuni za Bunge
Maalumu la Katiba, Tundu Lissu amesema ktendo cha Mwenyekiti wa Bunge la
Katiba kubadilisha kanuni kwa kutoa muda zaidi wa kuwasilishwa kwa
rasimu ya katiba, kinamkera.
Lissu alisema kitendo kama hicho ndicho
kilichomfanya yeye na mjumbe mwenzake, Ismail Jussa kutaka kujiuzulu
mara mbili kutokana na kupingana na wajumbe wenzao.
Akizungumza na gazeti hili jana mjini
hapa, Lissu alisema walitaka kujiuzulu kutokana na kuchoshwa na wajumbe
kufikia makubaliano ndani ya vikao, lakini wakitoka nje wanarudi na
mabadiliko.
“Tulikuwa hatusongi mbele tunafanya
uamuzi na kufikia makubalino, lakini wenzetu baadaye wanaenda
kujadiliana upya na kuja na mapendekezo tofauti na kuturudisha nyuma,”
alisema Lissu.
“Baada ya majadiliano yao, mimi na Jussa
tuliomba tujiondoe lakini walituomba tusijiuzulu kwa masharti kuwa
tunachokubaliana hawataweza kubadilisha.”
Alisema kile ambacho kimeanza kutokea
sasa ni kitendo cha Mwenyekiti Sitta kubadilisha kanuni ya 47 (a) ya
Bunge hilo juu ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kupewa muda
unaofaa kuwasilisha rasimu katika Bunge Maalumu la Katiba.
Lissu, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Singida Mashariki (Chadema), alisema pia hata kubadilisha kanuni kwa
kupokea kwanza taarifa ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na baadaye ndipo
Rais Jakaya Kikwete azungumze ni jambo wanalolipinga.
Home
»
»Unlabelled
» TUNDU LISSU:SITTA ANANITONESHA VIDONDA
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)


0 maoni:
Chapisha Maoni