Mbowe alisema kwa hali ilipofikia, kuna haja kwa
kila chama kuwapa semina wajumbe wake, ili walione Bunge hilo kuwa ni la
kitaifa na siyo kikao cha chama cha siasa.
“Kuzomeana ni mambo ya kitoto, siwezi kupongeza
utovu wa hali ya juu wa nidhamu ulioonyeshwa na baadhi ya wajumbe.
Tukiruhusu zomeazomea, itakuwa sawa na genge la wahuni,” alisema Mbowe.
Mbowe ambaye pia ni mjumbe wa Bunge hilo alisema,
kuna mambo ya msingi yanapingwa tu kwa sababu yametolewa na mjumbe
kutoka chama fulani cha siasa bila kuangalia mantiki ya hoja.
“Ni kweli kiti kinayumba nafasi ya kuchangia
inatolewa kwa upendeleo,lakini hiyo haiwezi kuwa sababu ya sisi
kushindwa kuheshimiana na kuheshimu mawazo ya wengine,”alisema Mbowe na
kuongeza;
“Kuna umuhimu wa vyama vyetu kurudi na kukaa na
wajumbe wetu kwa sababu mvutano mkubwa hauko kwenye lile kundi la watu
201 ni vyama vya siasa,”alisema
Kwa mujibu wa Mbowe,kama Bunge hilo halitatunga
kanuni kali ili kila mjumbe aheshimu mawazo ya wenzake na kuruhusu kila
mjumbe, aseme bila utaratibu ni vurugu.
Mbowe alisema kinachotokea ndani ya Bunge hilo kwa
baadhi ya wajumbe kufanya mambo aliyoyaita ni ya kitoto ikiwamo
kuzomea, ni kujidhalilisha na kushusha hadhi ya chombo hicho muhimu
Chanzo:- Mwananchi
Chanzo:- Mwananchi

0 maoni:
Chapisha Maoni