SALUM MKAMBALAWA CHANNEL TEN APATA AJALI YA GARI
Mtangazaji wa Channel Ten, Salum
Mkambala (pichani) amepata ajali ya gari ambalo alikuwa akiendesha
kutoka Dar es Salaam kuelekea Morogoro. Kwa mujibu wa mmoja wa
wafanyakazi wa Channel Ten ambaye amedokeza juu ya tukio hilo amesema
Mkambala alipata ajali hiyo maeneo ya Chalinze alfajiri ya leo na hali
yake inaelezwa kuwa ni mahututi baada ya kuumia vibaya. Haijafahamika
yuko hospitali gani kwani alikuwa peke yake kwenye gari na taarifa
ilitolewa na msamaria mwema kwa simu ya Salum na baada ya hapo simu yake
haipatikana tena.


0 maoni:
Chapisha Maoni