Mtoto Anastazia Jumanne (12) ambaye ni
mwanafunzi wa shule ya msingi katika wilaya na mkoa wa Geita amefanyiwa
ukatili wa kutisha baada kufungwa mpira kwenye pikipiki na baba yake
mzazi na kisha kuanza kumburuza mtaani.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea jana
majira ya sa tatu asubuhi katika moja ya mitaa ya mjini humo ambapo
inadaiwa kuwa binti huyo anayesoma darasa la nne katika shule hiyo
alikataa kwenda shule kitendo ambacho kilimkasirisha baba yake aitwaye
Jumanne Nkoyogi ambaye pia ni mfanyabiashara wa samaki mjini Geita.
mashuhuda wa tukio hilo baada ya kuona
asubuhi hiyo mtoto huyo akiburuzwa huku amefungwa kwenye pikipiki
walianza kupiga makelele na kukusanyana kwa lengo la kumkamata baba huyo
aliyekuwa anafanya unyama huo.
Baada ya kumkamata na kumtia kumtia
mikononi mwao walimpeleka kwenye ofisi ya sungusungu iliyopo Ihayabuyaga
kata ya Kalangalala na kufungiwa humo kwa usalama wake.
Akizungumzia tukio hilo katibu wa
sungusungu kata ya Kalangalala aliyempokea mtuhumiwa huyo Abel Richard
amesema tukio hilo liliwafanya wananchi kujaa jazba dhidi ya mzazi huyo
na kutaka kumpiga.
Amesema mzazi huyo kwa sasa anashikiliwa
na jeshi la polisi wilayani Geita baada ya katibu huyo kuwasiliana na
uongozi wa jeshi hilo na kuwatuma askari kwake kumchukua haraka kwa
usalama wake.
Afisa upelelezi wa mkoa wa Geita Simon
Pasua amekiri kuwepo kwa tukio hilo na kusema kuwa mtuhumiwa
anashikiliwa na jeshi la polisi hadi sasa kwa upelelezi zaidi.
Home
»
»Unlabelled
» UKATILI:MTOTO ABURUZWA NYUMA YA PIKIPIKI NA BABA YAKE KISA HAJAENDA SHULE
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)

0 maoni:
Chapisha Maoni