Mtoto aliyefariki baada ya kipigo hicho ni Vanesa Njojowa wa Kijiji cha Isisi wilayani Mbarali mkoani hapa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi
alisema tukio hilo lilitokea saa 5:00 usiku wa kuamkia jana baada ya
kuzuka kwa vurugu katika familia.
Msangi alisema baba wa marehemu ambaye ana umri wa
miaka 23 alizusha vurugu kubwa kwa mkewe na baadaye aliamua kutoa
kipigo kwa mtoto na kusababisha kifo.
Baba huyo anashikiliwa polisi wakati mwili wa marehemu ulitarajiwa kuzikwa jana baada ya polisi na madaktari kufanya uchunguzi.
Katika tukio jingine, Msangi alisema mtoto
anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka minne na mitano, Festo Mbiga
alifariki dunia baada ya kugongwa na lori eneo la Nsalaga Uyole jijini
hapa.
Mtoto huyo aligongwa juzi alipokuwa akikatisha barabara na kwamba polisi wanachunguza chanzo cha ajali hiyo.
Chanzo Mwananchi
Chanzo Mwananchi

0 maoni:
Chapisha Maoni