Ilielezwa kuwa Feng aliamua kujinyonga baada ya
nguzo za daraja alilokuwa akilisimamia katika ujenzi huo, kusombwa na
maji, jambo ambalo aliona kuwa limemvurugia kazi yake.
Baadhi ya watu waliokuwa jirani na kambi hiyo,
walisema baada ya kuharibika kwa kazi hiyo, wahandisi wenzake kutoka
China, walianza kumtenga hali iliyomfanya ajione kuwa mpweke na hatimaye
kuchukua uamuzi huo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Leonard
Paulo alisema tukio hilo lilitokea Jumamosi iliyopita ndani ya kambi ya
kampuni hiyo.
Alisema mwili wa marehumu ulikutwa ukining’inia
kwenye dari ndani ya chumba alichokuwa analala na kwamba polisi
wanaendelea na uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo.
Kamanda Paulo alisema baada ya kuchunguza mwili wa marehemu walikuta karatasi iliyokuwa imeandikwa ujumbe kwa lugha ya Kichina.
Alisema kwa kuwa hakuna mkalimani aliyekuwa jirani na eneo la tukio, polisi wanaendelea kumtafuta mtu wa kuutafsiri.
Alisema kwa sasa mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya St Francis iliyopo Kilakala, Morogoro.
Kivuko chazuiwa
Wakati huohuo, Halmashauri za Wilaya za Kilombero
na Ulanga kwa pamoja zimeamua kusimamisha kwa muda usiojulikana matumizi
ya Kivuko cha MV Kilombero Two kuvuka Mto Kilombero ambao umefurika
kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Kusimama kwa kivuko hicho kumesababisha baadhi ya wasafiri kukwama na wengine kulazimika kuvuka kwa kutumia mitumbwi.
Huduma pekee ya usafiri kwa sasa treni ya Tazara ambayo inafanya kazi mara moja kwa wiki.

0 maoni:
Chapisha Maoni