Hemedy
PHD na muigizaji mkongwe Tanzania King Majuto wameshuti filamu yao mpya
ya comedy kwa mara ya kwanza jijini Mwanza. Filamu walioipa jina la
‘Kimbulu’.
Hemedy
ameuambia mtandao wa Bongo5 kuwa wameamua kushuti filamu hiyo jijini
Mwanza ili kubadili mazingira na kuleta muonekano tofauti na ule wa Dar
unaoonekana kwenye filamu nyingi.
“Watu
wengi wamekuwa wakisema wamechoka kila siku kuona majengo ya Dar es
Salaam, kwa hiyo tumeamua kubadilika kuja huku halafu Mwanza yenyewe sio
town ni kidogo nje ya mji. Nafikiri kutokana na mandhari ya Mwanza mawe
mawe mtu atakuwa anajua kabisa kwamba project imefanyika ndani ya Rock
City.” Amesema Hemedy.
Ameelezea
kuwa filamu hiyo inahusu vijana wawili ambao walikuwa wameenda kijijini
kwa lengo la kutafuta vijana wanaojua kuigiza ili wawaunganishe na
wasanii wakubwa wa mjini lakini mwisho wa siku vijana hao wageuka na
kuendekeza uzinzi na kuwa wezi.
Vijana hao waliishia kwenye mikono ya wanakijiji waliowashambulia kwa kipigo kikali baada ya kukamatwa wakiiba kuku.
Amesema
lengo la kuigiza filamu hiyo ni kufikisha ujumbe kwa wasanii wenzao
kuwa kama wanaamua kusaidia watu wafanye hivyo na si vinginevyo.
“Kwa
hiyo ni kuwafungua macho wale wote wanaotumika kwa style hiyo, na
vilevile kuonesha wasanii kwamba kama tunaamua kusaidia tusaidie kweli
na isiwe na isiwe watu tunawafanyia michezo mibaya kama hiyo.”

0 maoni:
Chapisha Maoni