RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), Jamal Malinzi amesema hatajiuzulu nafasi ya Mwenyekiti wa Chama
cha Soka Mkoa wa Kagera (KRFA) pamoja na kuwa na majukumu ya kitaifa.
Katika taarifa yake aliyoitoa mbele ya
wajumbe wa mkutano mkuu wa KRFA mkoani hapa juzi Jumamosi, Malinzi
alisema wakati anakuja kuhudhuria mkutano huo alikuwa na wazo la
kujiuzulu.
Hata hivyo aliwaeleza wajumbe hao kuwa
ameachana na wazo la kujiuzulu nafasi ya uenyekiti wa KRFA, kwa kuwa
aliombwa na wajumbe asichukue hatua hiyo.
Alisema baadhi ya wajumbe wa KRFA
walitishia kuachia nafasi zao endapo angejiuzulu nafasi yake ndani ya
chama hicho ili aendelee kutumikia nafasi moja ya Rais wa TFF.
Pia alisema ameamua kuendelea ili kuzima
uvumi kutoka kwa wadau mbalimbali wa soka waliodai kuwa aligombea
nafasi ya uenyekiti wa KRFA ili apate tiketi ya kugombea kiti cha urais
wa TFF.
Katika hotuba yake kwa wajumbe hao
Malinzi aliwataka kuhakikisha wanashirikiana na halmashauri za wilaya
ili kutenga maeneo ya viwanja vya michezo na kusema Uwanja wa Kaitaba
utawekewa nyasi bandia baada ya kupata ufadhili wa Shirikisho la Soka la
Kimataifa (Fifa).
SOURCE: MWANASPOTI
Home
»
»Unlabelled
» JAMAL MALINZI AGOMA KUJIUZULU UENYEKITI WAKE
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)


0 maoni:
Chapisha Maoni