Raisi Jakaya Kikwete alipomtembelea kumjulia hali bilionea
kijana anayemiliki kampuni ya uuzaji na usambazaji wa vifaa vya
nyumbani ya Home Shopping Centre ya Kariakoo jijini Dar es Salaam, Said
Saad Mohamed .
Habari za uhakika kutoka chanzo makini
ambacho pia kipo karibu na familia hiyo ya kitajiri zinasema baada ya
kukamilika kwa matibabu yake yaliyoanzia nchini Afrika Kusini na baadaye
Ujerumani na kupona, mfanyabiashara huyo aliamua kuhamishia maskani
yake kwenye Jiji la Dubai ambao ni mji mkuu wa Muungano wa Nchi za
Kiarabu (United Arab Emirates).
Kule inasemekana bilionea huyo licha ya kuwa na biashara anamiliki nyumba.
KISIKIE CHANZO CHETU
“Said hakai tena hapa Bongo, amehama yeye na familia yake, hivi sasa anaishi Dubai. Unajua anaogopa kuendelea kuishi hapa baada ya lile tukio, ameona anaweza kuuawa maana hajui nani ni adui nani rafiki, huwa anakuja mara mojamoja, anakaa siku mbili tatu anaondoka zake,” kilisema chanzo hicho.

NI UAMUZI WA FAMILIA
Inadaiwa kuwa baada ya kutibiwa Afrika Kusini na kisha Ujerumani ambako alifanyiwa upasuaji wa mafanikio wa macho yaliyokuwa yameathiriwa na tindikali hiyo, familia ilikaa chini na kuamua kwamba ndugu yao asikae tena Tanzania.

“Kama suala ni biashara, hata Dubai ana
biashara, tena kubwa tu, sasa kwa nini asikae huko ambako ni salama
kuliko hapa? Kule ana nyumba nzuri na maisha ni mazuri, jamaa hawezi
tena kurudi na kuishi hapa, kimsingi amehama kimoja,” kilisema chanzo
hicho.
Jitihada za kumpata bilionea huyo
kupitia namba zake za simu za siku za nyuma zilishindikana, kwani zote
hazikuwa hewani, lakini mtu mmoja wa karibu na familia hiyo maarufu
zaidi Kariakoo, alithibitisha kuhama kwa mfanyabiashara huyo, Mtanzania
mwenye asili ya Yemen.
KUMPATA MSEMAJI WA FAMILIA NI KAZI KUBWA
Uchunguzi zaidi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, usiri umetawala kwenye familia ya bilionea huyo ambapo kumpata msemaji imekuwa kazi kubwa.
Uchunguzi zaidi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, usiri umetawala kwenye familia ya bilionea huyo ambapo kumpata msemaji imekuwa kazi kubwa.
“Unajua yaliyotokea ndiyo yametoa
fundisho, huwezi kumpata mtu akasema chochote kuhusu Said kwani kila mtu
anaogopa, maana unaweza kusema huyu ni rafiki kumbe ni adui mkubwa,”
kilisema chanzo.
MTUHUMIWA BADO KUKAMATWA
Kwa mujibu wa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi, Kinondoni, Dar es Salaam, ACP Camillius Wambura alisema juzi kwamba mpaka sasa hawajafanikiwa kumpata mtuhumiwa.
“Kusema kweli sina taarifa kama kuna mtu aliyekwishakamatwa kuhusiana na kummwagia tindikali huyo bwana,” alisema Wambura.

TUJIKUMBUSHE
Said alimwagiwa tindikali Julai 19, mwaka huu, mishale ya saa 2 usiku akiwa kwenye moja ya maduka yake yaliyopo kwenye jengo analodaiwa kulimiliki la Msasani Mall jijini Dar es Salaam.
Ilielezwa kuwa baada ya kumwagiwa tindikali alikimbizwa kwenye Hospitali ya Ami Wellness Centre iliyopo Masaki, Dar lakini ndani ya kipindi kisichozidi dakika 60 alichukuliwa na kupandishwa ndege kupelekwa nchini Afrika Kusini.

“Sehemu ya usoni kushuka kifuani upande
wa kulia na mkono wenyewe wa kulia ndiyo maeneo katika mwili wa ndugu
yetu yaliyoathirika zaidi na tindikali,” alisema ndugu huyo wa ndani
kabisa kwa sharti la kutotajwa jina, akaongeza:
“Jicho la kulia lenyewe lilipata athari
kidogo, kwani inaonekana wakati mmwagaji akifanya kile kitendo, yeye
alifumba macho kwa hiyo tindikali haikuingia ndani ya jicho.
“Ila kwa vile tindikali ilimwagika kwa
wingi juu kwenye jicho la kulia na kutokana na ukali wa tindikali
aliyomwagiwa, imesababisha kutengenezwa kwa mtoto wa jicho kwa hiyo
hawezi kuona mbali.
“Uamuzi wa kumpeleka Ujerumani ulifikiwa
baada ya kujiridhisha kwamba kule kuna wataalamu kuliko Afrika Kusini.
Oparesheni ya uso kubadili ngozi iliyoathirika, vilevile kufanya
upasuaji wa jicho na kuliweka sawa ni mambo ambayo tulijiridhisha
yanawezekana Ujerumani.”
NYUMBANI KWAKE KARIAKOO
Juzi, Uwazi lilifunga safari hadi kwenye nyumba ya bilionea huyo, Kariakoo lakini hakukuwa na ushirikiano wowote kutoka kwa mtu aliyedai ni mlinzi wa nyumba hiyo.
Chanzo Tuangaze Bongo blog
Juzi, Uwazi lilifunga safari hadi kwenye nyumba ya bilionea huyo, Kariakoo lakini hakukuwa na ushirikiano wowote kutoka kwa mtu aliyedai ni mlinzi wa nyumba hiyo.
Chanzo Tuangaze Bongo blog

0 maoni:
Chapisha Maoni