About

www.facebook.com/archileusanatory/pambazuabongo


Mwarobaini (Azadirachta indica) ni mti unaofahamika kwa uwezo wake wa kutibu magonjwa ya aina mbalimbali. Inaaminika kuwa mti huu umetoka huko India na Burma . Mwarobaini hushamiri zaidi katika nchi za tropiki na una uwezo mkubwa wa kuhimili ukame. Nchini Tanzania, mti wa mwarobaini huweza kupatikana kwa urahisi kabisa katika maeneo mengi ya mijini na vijijini. Jina “mwarobaini” linatokana na imani kuwa mti huu una uwezo wa kutibu magonjwa yapatayo arobaini. Majani na mbegu za mwarobaini vimekuwa vikitumiwa kama tiba kwa miaka maelfu katika nchi mbalimbali duniani. Kati ya magonjwa ambayo mti huu umetumika kutibu au kupoza ni pamoja na matatizo ya kusaga chakula tumboni, kisukari, kansa, magonjwa ya ngozi, malaria, ukungu (fungus), n.k. Matawi yake hutumiwa kama mswaki na magome yake hutumiwa kama dawa ya kusafisha meno. Mafuta ya mibegu ya mwarobaini hutumika kutengenezea vipodozi na sabuni. Kiziduo cha mibegu au mafuta yake hutumiwa kama dawa ya kuulia wadudu wanaoharibu mimea shambani. Tumekwisha ziona faida mbalimbali za mti wa mwarobaini, leo nitakufundisha namna ya kutumia mti wa mwarobaini kujitibu magonjwa ya ngozi.

 MAHITAJI :
 i. Majani ya mti wa mwarobaini. ii. Sufuria iii. Mwiko iv. Jiko la gesi, mkaa au jiko la mafuta.

HATUA ZA KUFUATA: 

1. Chukua majani mabichi ya mti wa mwarobaini na uyaweke kwenye sufuria. 
2. Chukua sufuria yako yenye majani ya mti wa mwarobaini na ui injike kwenye jiko lenye moto wa wastani. 3. Chukua mwiko wako na uanze kuyakoroga majani yako taratibu hadi yakauke bila kuungua. Majani yako yakiisha kauka, ipua sufuria yako, chukua majani yako yaliyo kauka, yasage kisha hifadhi unga unga wako kwenye chombo cha plastiki.

MATUMIZI :
 Tumia vijiko viwili vya chai kwenye kikombe cha robo lita chenye maji ya moto, mara mbili kwa siku kwa muda wa siku ishirini na moja. UTAPATA MATOKEO MAZURI SANA. NGOZI YAKO ITAKUWA LAINI, NYORORO NA YENYE NGOZI NYORORO

0 maoni:

Chapisha Maoni

 
Top