About

www.facebook.com/archileusanatory/pambazuabongo

 
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema madai kwamba yeye ni tajiri hayana ukweli wowote. Amesema yeye ni mfugaji na anamiliki ng’ombe zaidi ya 800 katika Jimbo la Monduli, mkoani Arusha.
Lowassa alisema hayo katika mahojiano maalumu yaliyofanyika ofisini kwake wiki iliyopita mjini Dodoma.
“Haya madai hayana hata chembe ya ukweli hata kidogo, isipokuwa mimi nadhani wananitakia mema kwa sababu ukiona jumba zuri wanasema la Lowassa, gari nzuri la Lowassa, kitu chochote kizuri wanasema cha Lowassa,” alisema na kuongeza:
“Wamesema uongo mwingi sana, mimi nasema tu nilichopata nimepata na sina utajiri kiasi hicho, lakini si mbadhirifu wa haki zangu ninazopata kama mshahara na haki nyingine.”
Alipotakiwa kutaja mali anazomiliki, Lowassa alisema: “Mimi ni mfugaji, nina ng’ombe zaidi ya 800 jimboni kwangu Monduli.”
Lowassa ambaye pia ni mbunge wa Monduli, alisema madai kwamba anamiliki utajiri uliopindukia yalianza kabla hajajiuzulu uwaziri mkuu na ilielezwa kuwa “maduka fulani” ni yake.
Alibainisha kuwa hata kampuni ya Alphatel ambayo wanamiliki kwenye familia yake iliwahi kuhusishwa na jengo kubwa lililojengwa na mtu mmoja mwenye asili ya Kiasia wilayani Kinondoni, Dar es Salaam likiitwa Alpha.
“Ikaonekana ni jengo langu, kule Mbezi kuna rafiki yangu mmoja walienda watu wakasema hii nyumba ya Lowassa. Yule bwana alitoka na bastola akawakimbiza. Mimi sina nyumba maeneo hayo,” alisema Lowassa.
Chanzo: Mwananchi.

0 maoni:

Chapisha Maoni

 
Top