Moshi. Mtalii mmoja raia wa Ujerumani, Jeane
Traska (32) amenasa katika miamba ya kilele cha Mawenzi cha Mlima
Kilimanjaro baada ya kwenda kinyemela eneo hilo ambalo haliruhusiwi
kupandwa na watalii isipokuwa kwa ruhusa maalumu.
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro
(Kinapa), Erastus Lufungilo, alilithibitishia gazeti hili jana kuhusu
kunasa kwa mtalii huyo pamoja na mwongoza watalii (Guide) aliyejulikana
kwa jina la Athman Juma kutoka Kampuni ya Nordic Tours.
“Ni kweli kuna tukio hilo na wote wawili wamenasa
huko tangu asubuhi na tunafanya kila jitihada kuokoa maisha yao, lakini
kimsingi walikwenda huko kinyemela kwa sababu wao walitakiwa kwenda Kibo
lakini wao wakaenda Mawenzi, alisema.
Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa
Nchini (Tanapa), Paschal Shelutete, aliliambia gazeti hili jana kuwa
mtalii huyo pamoja na mwongozaji huyo wa watalii wamenasa katika miamba
ya kilele hicho baada ya kamba waliyokuwa wakiitumia kunasa kwenye
miamba.
Shelutete alisema mtalii huyo alianza kupanda
mlima huo Machi 18 mwaka huu kwa kutumia njia ya Rongai, safari ambayo
ingewachukua siku tano, lakini kwa sababu ambazo hazijulikani alibadili
njia na kuelekea kilele cha Mawenzi badala ya Kibo.
“Tanapa kwa kushirikiana na kampuni yaNordic Tours
tunaendelea na jitihada za kuwaokoa kwa kutumia askari wetu wazoefu
pamoja na helkopta itakayosaidia zoezi la uokoaji kwa kutegemea hali ya
hewa itakavyotulia. Sasa hivi kuna mawingu mazito”alisema.
Kwa mujibu wa Shelutete, ili mtalii aweze
kuruhusiwa kupanda kilele hicho cha Mawenzi ambazo ni miamba, hutakiwa
kujaza fomu maalumu ili aweze kubeba dhamana yako mwenyewe endapo
utapatwa na matatizo katika kupanda kilele hicho.
CHANZO Mwananchi
CHANZO Mwananchi
0 maoni:
Chapisha Maoni