About

www.facebook.com/archileusanatory/pambazuabongo

Navi Pillay 
Mkuu wa tume ya haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay
Kamishna wa tume ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu ametoa taarifa za kutisha na kuhuzunisha kuhusu ghasia za hivi karibuni katika Jamuhuri ya Afrika ya kati , baada ya kutembelea taifa hilo kwa siku tatu .
Navi Pillay amesema watoto katika taifa hilo wamekuwa wakikatwa katwa vipande na wauaji wamekuwa wakila nyama ya watu wanao wauwa.
Aliongeza kusema kuwa chuki baina ya jamii zimefikia kiwango cha kutisha, na kwamba watu wamekua wakiteswa na kuchomwa .
Hata hivyo amesema kupelekwa huko kwa vikosi vya Ufaransa na Afrika kumepunguza kiwango kikubwa cha mauaji kwa sasa.
Jamuhuri ya Afrika ya Kati ilitumbukia katika limbo la ghasia baada ya waasi kuchukua mamlaka mwezi Machi mwaka jana.

CHanZo BBC

0 maoni:

Chapisha Maoni

 
Top