NYOTA wa sinema za Bongo,
Wastara Juma ameibuka na kusema kuwa, kuna mwanaume asiyependa mafanikio
yake kiasi kwamba alifurahia alipopata ajali na kuvunjika mguu, mumewe
Juma Kilowoko ‘Sajuki’ kufariki dunia na akatangaza kwamba, mwanaume
yeyote atakayemuoa atakufa kama Sajuki.
Katika mahojiano maalum na gazeti hili juzi, Bamaga - Mwenge, jijini Dar es Salaam, Wastara alisema mwanaume huyo aliwahi kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi miakka ya nyuma, wakamwagana.
Wastara aliyasema hayo baada ya kupigwa swali kwamba, kuna madai kifo
cha mumewe, marehemu Sajuki kilikuwa na mkono wa mwanaume aliyewahi
kuwa mpenzi wake (jina tunalishikilia kwa sasa).
“Ni kweli kuna mwanaume niliwahi kuwa na uhusiano naye, alitangaza kwamba yeyote atakayenioa atakufa kama aliyokufa Sajuki.
“Ukiachana na Sajuki, nilipopata ajali mwaka 2009 nikavunjika mguu na
kukatwa, huyo mwanaume ambaye tulishaachana siku nyingi, alitangaza kwa
watu kwamba yeye alitaka nivunjike miguu na mikono yote ili niwe kama
boksi,” alisema Wastara huku akilengwa na machozi.
Risasi Jumamosi: Sasa Wastara, kama hali ni hiyo wewe ulichukua uamuzi gani?
Wastara: Nilikwenda kumripoti Kituo cha Polisi Oysterbay (jijini Dar).
Risasi Jumamosi: Okay, lakini unaonaje madai kwamba, huyo mtu anahusika na kifo cha Sajuki?
Wastara: Kusema kweli mimi siwezi kujua maana Sajuki aliumwa namuona,
akazidiwa ikafika mahali Mungu akamchukua. Sasa kama ni mkono wa huyo
mwanaume sijui ila ilivuma hivyo.
Risasi Jumamosi: Lakini kwa tangazo lake hilo, wewe umejipangaje? Maana wanaume watakuwa wanakuogopa!
Wastara: Kama yeye amejipanga iwe hivyo, hata mimi nimejipanga pia.
Sina wasiwasi, lakini namtangaza huyo mwanaume kama adui yangu namba
moja. Sina wasiwasi, siwezi kudhurika na wala mwanaume atakayenioa
hawezi kudhurika.
Hayo ni maneno yake, akae nayo tu. Kama anataka vita, nipo tayari
lakini siku zote mimi ni mkimya ila mtu akinikorofisha huwa nacharuka
hasa.
Risasi Jumamosi: Tangu mmeachana na huyo mwanaume umewahi kukutana naye popote?
Wastara: Sikumbuki kwa kweli. Nadhani sijawahi kumwona ila yupo. Amekuwa adui hata wa familia ya kwetu kwa ajili ya matamshi yake hayo.
Risasi Jumamosi: Kwani kuachana kwenu kulitokana na nani?
Wastara: Mimi nilimchoka kwa tabia yake. Alikuwa hajatulia. Mbaya zaidi
manyanyaso yalikuwa kila siku. Sijawahi kufurahia uhusiano wangu na
yeye.
-GPL
Home
»
»Unlabelled
» DUH! ATAKAYEMUOA WASTARA ATAKUFA KAMA SAJUKI...KISA NA MKASA..CHEKI HAPA
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 maoni:
Chapisha Maoni