Walimui zaidi ya 350 wa shule za msingi na sekondari waliopangiwa kufanyakazi ya kufundisha katika halmashauri ya wilaya ya kigoma wamepokelewa kwa mbwe mbwe na bashasha huku wakipewa motisha mbali mbali kwa kuwahamasisha kufanya kazi kwa bidii hatua inayotarajia kuinua kiwango cha elimu wilayani humo na mkoa wa kigoma kwa ujumla kwa mpango wa matokeo makubwa sasa.
Walimu
hao wamepewa vitu mbali mbali nje ya utaratibu wa kawaida wa serikali
kwa watumishi wake ikwemo kupatiwa magodoro, taa kwa kila mmoja na pesa
ya ziada ya kujikimu
Ikiwa ni wiki ya elimu kwa halmashauri zote
nchini, walimu waliopangiwa kufanyakazi ya kufundisha katika
halmashauri ya wilaya ya Kigoma wamepokelewa kwa mbwe mbwe kuanzia
kwenye kituo cha mabasi kigoma mjini kwa magari ya halmashauri na wadau
mbali mbali wa elimu mkoani hapa.
Walimu hao wameeleza kuwa ni
jambo la pekee kwa halmashauri hiyo ambalo linapaswa kuigwa na
halmshauri zote nchini huku wakisisitiza kuwa heshima ya walimu inapaswa
kurudi.
Kwa upande wao viongozi wa halmashauri ya kigoma
wameeleza jinsi ambavyo wamejipanga kuhakikisha mwalimu anapata huduma
inayostahili.
Afisa elimu wa mkoa huu ametoa onyo kwa walimu
waliobainika kutaka kuajiriwa kinyemela ndani ya halmashauri hii kwa nia ya
kufuata motisha.
Kukabidhiwa kwa vifaa hivi vinawapa hamasa
walimu kueleza jinsi walivyojipanga kuhakikisha wanafanyakazi kwa bidii
ili kuinua kiwango cha elimu.
Kigoma ni miongoni mwa mikoa
iliyofanya vibaya kwa matokeo ya mitihani ya kumaliza elimu ya darasa
la mwaka 2013 huku serikali ikiajiri walimu wengi mwaka huu ambapo kwa
halmashauri ya wilaya ya kigoma hadi sasa walimu zaid ya 350 kati ya
420 wameripoti na tayari wanapelekwa katika vituo vyao vya kazi.
0 maoni:
Chapisha Maoni