Watanzania wanne waliojeruhiwa katika
mlipuko wa bomu katika ubalozi wa Marekani mwaka 1998 na wengine watano
waliofariki dunia katika mlipuko huo watalipwa fidia ya Sh672 bilioni,
kiwango ambacho ni sawa na bajeti ya wizara nne za Tanzania.
Watanzania hao waliuawa na wengine
kujeruhiwa katika moja ya mashambulizi pacha yaliyotokea kwa wakati
mmoja jijini Dar es salaam na Nairobi, Kenya na ambayo yaliratibiwa na
Osama Bin Laden akitumia mtandao wa kundi la Al Qaeda mwaka 1998 kwenye
ofisi za balozi za Marekani.
Katika mashambulizi hayo yaliyotokea saa
4:00 asubuhi Agosti 7, 1998, Wakenya 200, Watanzania 10 na Wamarekani
12 walipoteza maisha na pia magaidi wawili nao walikufa.
Kati ya Watanzania 10, ni kesi za watu wanne tu waliouawa tu zilizofunguliwa kudai fidia ya watu hao kupoteza maisha.
Home
»
»Unlabelled
» WATANZANIA WALIOLIPULIWA NA OSAMA KULIPWA Sh 672 BILION
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 maoni:
Chapisha Maoni