Jana
September 5 2014 kwenye eneo la Sabasaba hapa Musoma ilitokea ajali
mbaya sana ya mabasi mawili yakiwa na abiria na kulihusisha gari jingine
dogo ambapo majeruhi ni zaidi ya 70 na waliofariki ni 39 Wanawake kwa
Wanaume kwa mujibu wa taarifa mpya za vifo zilizotoka muda mfupi
uliopita.
Kwa kuguswa na tukio hili waziri wa uchukuzi Dr. Harryson Mwakyembe
ilibidi aahirishe ratiba zake nyingine na kulazimika kuja Musoma
kuwatembelea majeruhi leo asubuhi kwenye hospitali ya mkoa pamoja na
kwenda kwenye eneo la ajali kutazama.
Baada ya hapo Waziri Mwakyembe akaongea na millardayo.com na kueleza yafuatayo >> ‘Inabidi
niwape pole Watanzania wote ambao wamepoteza ndugu jamaa na marafiki,
taarifa za ajali nimezipata nikiwa Dodoma kwenye bunge maalum ikawa sasa
nitafikaje haraka Musoma kwa hiyo ikabidi nitafute ndege leo asubuhi
kuja hapa’
Kuhusu
Wasanii wa bongofleva na Clouds Media Group kufanya maamuzi ya
kuahirisha tamasha ambalo lilikua lifanyike jana hapa Musoma, Waziri
Mwakyembe amesema >> ‘hii
imenifurahisha sana… inaonyesha Utanzania tulionao Watanzania, ni
vizuri wamefanya hivyo na ninawapongeza sana Clouds Radio kwa kuguswa na
maswala ya jamii’
‘Ajali sasa hivi Tanzania zimechukua nafasi ya yale magonjwa
tunayoyaogopa hasa kwa kuchukua maisha ya watu na kujeruhi na kuiingizia
serikali gharama kubwa ya matibabu, hatuwezi kuliangalia hili swala
hivihivi mimi kama Waziri wa uchukuzi nimewaambia wenzangu kuanzia sasa
Watanzania wataona mabadiliko makubwa’ - Dr. Mwakyembe
- Tunaanza na hawa waliopata ajali, nimeelekeza na najua vyombo vinavyohusika Polisi pamoja na SUMATRA watatekeleza… kwanza kuzifungia kampuni za haya mabasi ya J4 na Mwanza Coach wasijihusishe na usafirishaji wa abiria tena, hatuwezi kuwa tunapata ajali za kijingajinga namna hiyo, nimeliona eneo lenyewe liko wazi kabisa lakini ni watu tu wameamua, dereva wa huku anamuona mwenzake na kusema mimi lazima anipishe’ – Dr. Mwakyembe
- Tumeelekeza Wafanye uhakiki wa madereva wao wote na tunahitaji picha zao lakini vilevile tunahitaji mikataba ya kazi, hatutaki mabasi ya kupeleka abiria yaendeshwe na watu tu kwa majaribio, nataka ushahidi wa kila dereva kwamba amejiunga na hii mifuko ya akiba ya Wafanyakazi, tuone kabisa mchango wa Mwajiri na mfanyakazi kila mwezi’
- Nimeagiza lazima tuangalie BIMA ya hiyo gari, unajifikiria mwenyewe tu ukipoteza gari ulipwe kidogo gari yako lakini hufikirii kuhusu binadamu…. bila comprehensive haendeshi mtu gari kuchukua abiria.
Tamasha la Fiesta lililokua lifanyike Ijumaa hapa Musoma sasa imefahamika litafanyika Jumapili ya kesho September
7 2014 ambapo pia imehamasishwa kwa wingi watu kujitokeza ili mapato
hayo yapelekwe kwa ndugu waliopoteza watu na majeruhi ajalini.
0 maoni:
Chapisha Maoni