About

www.facebook.com/archileusanatory/pambazuabongo

Tukio katika picha ni mkuu wa wilaya ya Mbulu anayetajwa kugombea ubunge tena hapa Biharamulo Bwana Anatory Choya.
Tukio hilo la kusikitisha lilijitokeza baada ya wananchi wa kijiji cha Hydom kupinga agizo la Choya, lililowataka kufanya uchaguzi wa kaimu mwenyekiti wa kijiji hicho, kabla ya kufanya uchaguzi mdogo, ambapo walipinga kwa kudai kuwa hakuna sheria hiyo. Mmoja wa wananchi hao alilumbana na mkuu huyo wa wilaya mbapo Choya alijibu; “Nami nitarudi kwetu."
Naye Tikin akasema tena: “Unasema utarudi kwenu
Biharamulo wakati hawakutaki kwani ulifukuzwa
ubunge?”
Maneno hayo yalionyesha kumkwaza Choya ambapo alipiga magoti huku machozi yakimlenga na kumwomba Mungu afanye jambo kwa watu wa Haydom kwani wanamdharau kabla ya kujitokeza wazee watatu wa Haydom na kumwomba msamaha mkuu huyo wa wilaya.

Je,ataweza ubunge tena? Je,atapiga magoti na Biharamulo

0 maoni:

Chapisha Maoni

 
Top